22 Jan 2020 Tukio Malengo ya Maendeleo Endelevu

Muongo wa kuchukua hatua za kuwezesha kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu

Malengo ya Maendeleo Endelevu ni muhimu duniani na yanaweza kuboresha maisha ya kila kiumbe ya siku za usoni. Yanashughulikia changamoto tunazokumbana nazo duniani ikiwa ni pamoja na umaskini, kubaguliwa, mabadiliko ya tabianchi, kuharibika kwa mazingira, changamoto za amani na haki. Malengo hayo 17 yanaingiliana, na ili kutopuuza lengo lolote, ni muhimu kuyafikia yote kufikia mwaka wa 2030.

Miaka mitano tangu kuzinduliwa kwake Muongo wa kuchukua hatua za kuwezesha kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu ni ishara ya kujitolea upya kwa jamii ya kimataifa kuimarisha juhudi zake ili kufikia malengo haya ya kimataifa.

Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) linatoa mchango kwa muongo huu kwa njia mbalimbali:

  • Mazingira yanategemea kila mojawapo wa malengo hayo 17- kuanzia na kutokomeza umaskini, kupunguza ubaguzi hadi kujenga jamii endelevu kote ulimwenguni. UNEP hushirikiana na wenzao wanaofanya kazi katika Mifumo ya Umoja wa Mataifa kukuza uwezo wa nchi kufuatilia kwa makini hatua zake za kufikia malengo wakiwa na lengo la kuhakikisha kuwa mazingira yanajumuishwa katika kila kipengele cha maendeleo endelevu.
  • UNEP hufuatilia hatua zilizopigwa kufikia malengo kupitia rasilimali kama vile jukwaa la World Environment Situation Room, jukwaa la kupata maarifa lililoundwa ili kukusanya, kufanyia kazi na kushiriki data muhimu za sayansi na utafiti unaohusiana na mazingira. Pia hushughulikia data nyingi mpya kutoka kwa sateliti, droni na kutoka kwa wanasayansi. Jukwaa hilo lina vifaa muhimu vya kutathmini hatua zilizopigwa ili kufikia malengo yaliyowekwa.
  • Jukwaa la UNEP linaloshughulikia masuala ya mazingira yanayohusu Sayansi, Sera na Biashara lilibuni kikundi cha kushughulikia data, kuichanganua na kutumia mitambo inayoweza kusoma (AI) mnamo Mechi mwaka wa 2018. Kupitia kikundi hiki, UNEP imekuwa ikifanya kazi kwa ushirikiano na wabia mbalimbali kutathmini jinsi ya kutumia data vizuri kufuatilia masuala ya mazingira ikiwa ni pamoja na malengo yaliyowekwa. UNEP pia inashirikiana na jamii ya kimataifa ya wanasayansi ili kutafuta mbinu mpya ya kutumia data mpya kujenga Mfumo wa Ekolojia wa Kijidijitali wa Mazingira.
  • Kupitia uchunguzi wa mara kwa mara kupitia Foresight Briefs na ripoti inayotolewa kila mwaka ya Frontiers report, UNEP huuanisha mambo msingi yanayojitokeza kwa mazingira kote ulimwenguni, ikiwa ni pamoja na yale yanayohusiana na utekelezaji wa malengo yaliyowekwa.
  •  Taarifa za Sera za Malengo ya Maendeleo Endelevu inaonyesha vitu vinavyohitaji kufaywa ili kuleta mabadiliko kwa mazingira. Ushahidi uliopo hutokana na data ya kisayansi na taarifa kutoka kwa World Environment Situation Room pamoja na visa kutoka kwa eneo husika.
  • UNEP hutoa ushauri wa kiufundi na msaada wa jinsi ya kushughulikia mazingira. Pia hukuza sheria na mikakati zinazoongoza nchi hizo kuzitekeleza kikamilifu. Mfano mmoja ni kazi ya mipango ya hatua za mkakati wa kitaifa wa bayoanuai.
  • Huku asilimia 70 ya misitu duniani ikiwa hatarini kuangamia, UNEP iko mstari mbele kwa ushirikiano na taasisi nyinginezo za Umoja wa Mataifa kutoa wito kwa watu wote kutilia maanani kilimo kinachojali mazingira; kuwa na mfumo wa usambasaji wa bidhaa usio chafua mazingira; kutumia bidhaa kwa njia endelevu; kushirikiana na sekta za kibinafsi; na kuwatoza fedha wanaotumia kaboni.
  • Suluhu inayojali mazingira ni mojawapo wa njia mwafaka za kuwa na maisha mazuri, kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kutunza sayari. UNEP na wabia wenza pia wanasimamia Muongo wa Kuboresha Mifumo wa Ekolojia wa mwaka wa 2021 hadi 2030. Muongo huu unanuia kukusanya njia za sayansi na namna nzuri ya kuboresha mifumo ya ekolojia na kuchochea uchukuaji wa hatua.
  • UNEP huleta wanasayansi na waunda sera pamoja kila baada ya miaka kadhaa katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa. Kauli mbiu ya Mkutano Mkuu ujao utakaotokea mnamo Februari  mwaka wa 2021 Kuimairisha Juhudi za Kushughulikia Mazingira Kuyafikia Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Tuna miaka 10 ya kuleta mabadiliko duniani Haiwezekani kuendelea na mienendo ya kawaida iwapo tunataka kufikia malengo yetu.

image
Wavuvi nchini Liberia. Maisha ya zaidi ya watu bilioni tatu hutegemea bahari na bayoanuai ya maeneo ya pwani. Maji ya maeneo ya pwani yanaendelea kupungua kutokana na uchafuzi na urutubishaji. Bila juhudi za kutosha, urutubishaji wa maeneo ya pwani unatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 20 kwa mifumo mikuu ya ekolojia kufikia mwaka wa 2050. Kutoka: Ukweli na takwimu kuhusu bahari. Picha na UNEP-Ekonomia ya Mifumo ya Ekolojia na Bayoanuai

Kiongozi wa uhamasishaji

UNEP na wabia hufanya kampeni za kimataifa za mawasiliano ili kufikia malengo yake: Wild for LifeBreathelife na Clean Seas. UNEP pia hushirikiana na kikosi cha Mabalozi wa Nia Njema, Mashujaa na Viongozi kusambaza ujumbe kuhusu umuhimu wa kutunza na kuhifadhi mazingira. UNEP huendesha programu ya Mabingwa wa Dunia, ambayo ni programu ya kutoa matuzo katika nyanja ya mazingira ili kuenzi miradi mipya yenye manufaa kwa mazingira, na kuwatuza waanzilishi wake.

UNEP inafanya nini kuhakikisha masuluhisho yanapatikana haraka?

Mfano wa hivi majuzi ni kuwa UNEP ikishirikiana na MISHENI YA KUDUMU YA UJERUMANI walizindua Fursa za Kimataifa za Malengo ya Maendeleo Endelevu (GO4SDGs) wakati wa Mkutano Mkuu wa Malengo ya Maendeleo Endelevu uliotokea mjini New York mwezi wa Septemba mwaka wa 2019 ili kuimarisha juhudi na kuleta suluhu ya kuwezesha kufikia malengo yake. Watafikia waunda sera, biashara ndogondogo na biashara za kadiri na vijana. Idadi hiyo kubwa inalengwa kwa nia ya kuhamasisha watu kuunda chumi endelevu zisizo na ubaguzi katika ngazi zote.

GO4SDGs itategemea na kuongezea UNEP maarifa mengi ya kisayansi na kuyasambaza kupitia ushirikiano uliopo na kupitia programu zilizopo kama vile One Planet Network, Partnership for Action on Green Economy, Green Growth Knowledge Partnership, International Trade Union Confederation’s Just Transition Centre na UNEP Finance Initiative, huku wakihakikisha kuwa kila eneo lina njia ya kipekee ya kukabiliana na changamoto zinazotofautiana katika kila eneo duniani. Mradi huu pia utaanzisha ubia na mashirika yanayofanya kazi moja kwa moja na kampuni za biashara na sekta za binafsi ili kuharakisha uchukuaji wa hatua, ikijumuisha Jukwaa la Uchumi la Kimataifa.

UFADHILI

Hifadhi ya Vipimo vilivyotolewa na UNEP na Green Growth Knowledge Partnership inaashiria ongezeko la asilimia106 la ufadhili kwenye nishati isiyochafua mazingira kote ulimwenguni tangu mwaka wa 2015. Tulifaulu kupata maendeleo ya kupendeza wakati wa kikao kilichoandaliwa na Umoja wa Mataifa cha Net-Zero Asset Owner Alliance, ambapo miezi miwili baada ya mifuko mikuu 12 ya malipo ya uzeeni na makampuni za bima kujitolea kuepukana na hewa ya ukaa kufikia mwaka wa 2050, bidhaa wanazomiliki zimeongezeka na kufikia dola za Marekani trilioni 3.9.

Masuali kwa viombo vya habari na mahojiano, tafadhali wasiliana na: unenvironment-newsdesk@un.org