Picha: Unsplash
09 Jun 2022 Video Chemicals & pollution action

Uchafuzi wa plastiki: kemikali hatari katika plastiki zetu

Picha: Unsplash

Uzalishaji wa jumla wa plastiki duniani unakadiriwa kufikia tani milioni 34,000 kati ya mwaka wa 1950 na mwaka wa 2050.

Kemikali hatari zinazotolewa na bidhaa za plastiki katika kipindi chote zinapotumika zinaweza kuhatarisha maisha ya binadamu na mazingira, ikijumuisha pale ambapo taka haishughulikiwi ipasavyo na kujikuta hewani, majini na mchangani.  

Ijapokuwa maandalizi ya makubaliano jumuishi ya kisheria kuhusiana na uchafuzi wa plastikiyanaendelea, taka ya plastiki na kemikali katika plastiki ni masuala yanayojadiliwa katika mikutano ya 2021/2022 ya  makongamano ya Nchi Wanachama wa Makubalialo ya Basel, Rotterdam na Stockholm, ikijumuisha Jukwaa la Plastikikuanzia Juni 8 hadi 10, 2022 mjini Geneva, Uswizi.

Wataalamu wanasema kuwa hatua za dharura zinahitajika ili kuelewa vyema na kudhibiti matumizi ya kemikali hatari kwa kipindi kizima cha kuwepo kwa plastiki.

Katika video hii, tuangazia bidhaa za plastiki, kemikali ndanimwe na uwezekano wa kudhuru afya ya binadamu na mazingira.

 

 

 

Maudhui yanayokaribiana